Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa hana uhakika wa kufanya usajili mwingine kabla ya dirisha la usajili halijafungwa saa chache zijazo
Mourinho amekuwa akihitaji kumsajili beki wa kati wa Leicester City, Harry Maguire, Toby Alderweireld anayekipiga Tottenham Hotspur na Jerome Boateng ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.Lakini meneja huyo raia wa Ureno kupitia mkutano wake na waandishi wa habari mapema hii leo ameeleza kuwa kunauwezekano mkubwa wa kutoongeza mchezaji mwingine ndani ya kikosi chake kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo siku ya Alhamisi

